Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


SHUGHULI za Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zimeanza rasmi katika Ukumbi wa St. Gaspel mjini Dodoma ambapo wajumbe kutoka kanda 13 za shirikisho hilo hapa nchini, pamoja na wagombea wa nafasi mbalimbali wamehudhuria.


Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa na viongozi wa uchaguzi wa TFF kwenye mkutano huo.
Uchaguzi huo umetanguliwa na Mkutano Mkuu wa TFF ambao umezinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ukiwa na ajenda 14 zikiwemo kutambulisha wajumbe, kupitisha wagombea na ajenda ya uchaguzi.
Wajumbe wa mkutano huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano huo, Dkt. Mwakyembe amewasisitiza wajumbe wanaoshiriki uchaguzi huo kuzingatia kanuni za utawala bora ili kuleta tija katika maendeleo ya soka hapa nchini.
Hali ilivyokuwa ukumbini.

Waliohudhuria uchaguzi huo ni pamoja na Makamu Rais wa TFF, Wallace Karia, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Salum Madadi, pia wajumbe wa CAF na Fifa ambao wameona mchakato wa uchaguzi utachelewa kulingana na jinsi mipangilio yao ilivyo, hivyo na wao wameshauri mkutano ufanyike haraka ili waanze shughuli ya uchaguzi mara moja.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top