Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewataka wajumbe wa mkutamno mkuu wa TFF kuwa makini katika kufanya maamuzi ya kuwachagua viongozi wa Shirikisho hilo kwakuwa wao ndiyo tumaini la watanzania.
Mwakyembe ameyasema hayo mkoani Dodoma ambapo uchaguzi wa viongozi mbali mbali wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania unaendelea.
Katika uchaguzi huo wapo pia wageni kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani FIFA na lile la Afrika Caf wakiwa wanafuatilia kwa makini namna mchakato wa kupata viongozi wapya wa TFF unavyoendeshwa.
Dkt Mwakyembe amesema kuwa TFF inahitaji viongozi watakao walea watoto wenye vipaji vya soka walioibuliwa katika mashindano ya hivi karibuni na watakao weza kusimamia mfumo wa leseni za klabu.
“Ndugu wajumbe viongozi bora huibuliwa na wajumbe makini wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo usioteteleka kwa vishawishi vya mpito, serikali inaamini tuna wajumbe makini huku ndani wasioyumbishwa na vishawishi vya muda na vishawishi vya mpito, tunataka viongozi wanaongozwa na uzalendo wa hali ya juu, hivyo tunataka viongozi bora wa TFF wenye hali, moyo, uelewa, weledi na uadilifu unaotakiwa kupeleka soka letu mbele” alisema Mwakyembe


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top