Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Dennis Dillip ambaye ni Mjiolojia kuhusu mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni ya Sunshine Mining Limited uliopo Chunya wakati alipoutembelea 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakipata Maelezo kutoka kwa Afisa Madini wa Mkoa wa Mbeya Mhandisi Said Mkwawa kuhusu taarifa za Kampuni ya Sunshine Gold Mininga Limited wakati alipotembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni hiyo wilayani Chunya Agosti 1, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia wimbo maalum unaozungumzia utendaji wa serikali ya Awamu ya Tano ulioimbwa na Kwaya maarufu ya Kiwete katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Sabsaba mjini Chunya Julai 1, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sabasaba mjiini Chunya Agosti 1, 2017. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mkuki kutoka kwa Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaso ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa Chifu wa makabila ya Wakimbu na Wasafa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Chunya Agosti 1, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya SUNSHINE GROUP, Betty Mkwasa wakati alipotembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa Sunshine Mining Limited uliopo Chunya Agosti 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top