Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mmoja wa wananchi kutoka Wilaya ya Temeke (aliyesimama) akieleza kero yake kwa Mhe. Lukuvi wakati wa kusikiliza na kutatua kero za Sekta ya ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, amekutana na wakazi wa Wilaya ya Temeke na Kigamboni katika kusikiliza na kutatua kero za Sekta ya ardhi. Katika mahojiano na wananchi hao, Mhe. Lukuvi amewaonya wananchi kuwa makini na matapeli wanaochukua nyaraka halali za umiliki na kutengeza nyaraka feki.
Hayo yamebainika baada ya baadhi ya wananchi kulalamikia mmliki wa kampuni ya Holland Investment iliyopo jijini Dar es Salaam kwamba, amekuwa akichukua nyaraka halali za umiliki kwa wananchi kwa lengo la kuwasaidia na baadae kuwabadilishia na kuwarudishia nyaraka feki.
Mhe. William Lukuvi akisisitiza jambo kwa wananchi waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kutoa kero zao za masuala ya ardhi.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top