Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mchezajiwa Klabu ya Liverpool, Philippe Coutinho.
Kampuni ya Fenway Sports Group ambao ndiyo wamiliki wa Klabu ya Liverpool, wametoa tamko kuhusu tetesi za usajili wa mchezaji wao, Philippe Coutinho anayewaniwa na Barcelona.
Liverpool imekuwa katika presha kubwa kutokana na mchezaji huyo kuwania na wababe hao wa Hispania lakini Liverpool wamekataa dau la kumuuza mara tatu.Awali Barcelona ilikuwa tayari kutoa pauni 72m ili imsajili, baadaye ikatoa pauni milioni 80 na kisha pauni milioni 90 lakini zote hizo zimekataliwa na Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ambaye amesema kuwa Coutinho bado yumo kwenye mipango yake.Wamiliki hao wametoa tamko la maandishi kuwa hawana mpango wa kumuuza Coutinho kwa kiwango chochote kile.
Wamesema Hivyo baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa Barcelona wanataka kuweka pauni pauni milioni 100 ili kuongeza ushawishi wa kumsajili Coutinho.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top