Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa kanisani wakati wa ibada ya kuaga.
Watoto wa Marehemu
Watoto wa marehemu.
Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowass na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo wameungana na wananchi wa Arusha katika mazishi ya aliyekuwaya mfanyabiashara maarufu, Faustine Melleo Mrema yaliyofanyika Ngurudoto mkoani humo.

Waombolezaji wakiendelea kuaga mwili wa marehemu.
Maelfu ya waombolezaji wakiwemo viongozi wa madhehebu mbalimbali wa dini, wafanyabiashara wakubwa katika sekta ya utalii, wanasiasa, viongozi wastaafu ni miongoni waombelezaji waliomsindikiza tajiri huyo aliyeaga dunia akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini hivi karibuni.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiaga mwili wa mfanyabiashara Faustin Mrema katika ibada iliyofanyika katika hoteli ya Ngurudoto Arusha.

Mwili wake umepumzishwa katika eneo jipya la makaburi ya familia jirani na hoteli yake ya kitalii ya Ngurdoto Mountain Lodge iliyopo Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.


Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa akiteta jambo na katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakiteta jambo kwenye msiba wa mfanyabiashara Faustin Mrema

Katika mazishi hayo, Lowassa alimzungumzia marehemu kama mtu atakayekumbukwa kwa matendo yake ya kuwajali watu wanyonge.


Waombolezaji waliojitokeza katika ibada ya mazishi.

Kikwete ambaye hakuzungumza chochote alikua kivutio kwa viongozi na wananchi waliotaka kumsalimia lakini umati wa watu na ulinzi ndiyo vilikuwa vikwazo kwa wananchi huku muda wote akiwa katika hali ya maombolezo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiaga mwili  marehemu.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni waziri wa zamani wa mambo ya nje, Bernard Membe, waziri wa zamani wa fedha, Baziri Mramba, wabunge na wakuu wa wilaya.

Ndugu na marafiki wakiaga mwili.

Askofu Mkuu wa kanisa la International Evangelism, Dk Eliud Issangya aliyeongoza ibada hiyo amemzungumzia marehemu kama mtu aliyewapenda watu wote bila ubaguzi wa rangi wala kabila.

Alisema alikuwa ni mtu aliyependa kufanya kazi kwa bidii, hatua iliyompa utajiri mkubwa ambao aliutumia kuwasaidia wahitaji.


Ndugu na marafiki wakiaga mwili.

Mtoto wa kikewa marehemu, aitwaye Joan Mrema ndiye amepewa jukumu la kusimamia mirathi ya baba yake ambao ni hoteli za kitalii, kampuni za kitalii, maduka ya kubadilisha fedha na biashara nyingine.Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top