Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Vigogo watano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wanefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU wakidaiwa kuhujumu uchumi kwa kuisababibishia serikali hasara ya takribani Milioni 275.
Vigogo hao wa zamani waliyofikishwa Mahakamani ni pamoja na aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Lusekelo Kasanga, Mkurugenzi wa Fedha, Robert Shemhilu, Harun Mattambo, Godson Makia, Ofisa Ugavi,  msambazaji kutoka kampuni ya M/S Young Dong Electronic Co. Ltd Martin Simba pamoja na Mwanasheria wao.
Hata hivyo, Wakili wa serikali Vitalis Peter amewasomea mashtaka mawili ya uhujumu uchumi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba ambapo amedai kuwa kati ya Januari na Desemba 2011 katika Ofisi za Tanesco Ubungo, washtakiwa wakiwa waajiriwa wa Shirika hilo, walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji Martin Simba bila ya kufanya uhakiki na kuisababishia serikali hasara ya takribani Milioni 275.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top