Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baada ya kuachia ngoma yake mpya ‘Wale Wale’, Shetta amewajibu mashabiki wanaodai asikae kipindi kirefu bila kutoa ngoma.
Shetta ambaye alikaa zaidi ya miezi 10 bila  kutoa wimbo amesema atajaribu kubadilika lakini haamini katika kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja.
“Mimi naamini katika kitu ambacho nakifanya, nimeshauriwa nifanye back to back lakini hata hiyo itaongezeka ngoma moja au mbili, sidhani kama natakiwa nifanye vitu ambavyo watu wanasema au wanafikiri ni sawa, mimi natakiwa niamini katika kitu ambacho nafanya,” Shetta ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.
“Lakini kutokana mashabiki wanataka pia nafuata kile wanachopenda nitajaibu kubadilika ila katika moyo wangu siamini katika kutoka nyimbo nyingi. Bajeti pia huwa inabana kutokana kitu ninachotaka kukifanya pia ni kikubwa,” amesisitiza.
Katika hatua nyingine Shetta amesema kwa sasa ameshafanya video ya ‘Wale Wale, pia ameshalipia video ya project nyingine inayofuata.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top