Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mwanamitindo Hamisa Mobetto kwa siku za hivi karibuni amekuwa akiwapa mashabiki wake sababu za kumuongelea na hii ameendelea kuifanya baada ya karibuni kuchapisha picha zake zinazoonyesha kuwa ni mjamzito, na sasa swali limebaki ujauzito huo ni wa nani?


Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa ujauzito huo ni wa Majey ambaye ndiye baba wa mtoto wake wa kwanza na kwamba sasa wanategemea mtoto wa pili.

Lakini mbali na hao wanaodai kuwa ni mtoto wa Majey, wengine wanadai kuwa ni mtoto wa Diamond Platnumz licha ya kuwa mwanamuziki huyo amekanusha kuwa ujauzito huo si wa kwake, huku akimtaka Mobeto aseme ni ujauzito wa nani.

Kila mmoja amekuwa akisema lake, lakini anayejua ukweli kuhusu ujauzito huo, ni Hamisa Mobeto.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top