Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Timu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Singida United mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Mabatini ukiwa ni mchezo wa maandalizi ya msimu mpya unaotarajia kuanza Agosti 26.Ruvu walikuwa wa kwanza kupata bao likifungwa na Full Maganga dakika ya 20 hata hivyo goli hilo halikudumu kwani dakika ya 26 mshambuliaji wa zamani wa Jkt Ruvu Atupele Green aliweza kuisawazishia Singida hadi mapumziko timu hizo zilikwenda zikiwa zimefungana 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo hakuna timu ambayo iliweza kupata goli hadi dakika 90 kipyenga kinamalizika timu hizo zilitoshana nguvu sawa kwa kufungana goli 1-1.
Singida United wanatarajia kesho kuwasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Yanga mchezo ambao utapigwa siku ya Jumamosi na unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini kuona kocha wa zamani wa Yanga,Hans Van Der Pluijm anakutana na timu yake ya zamani ambayo ipo chini ya George Lwandamina.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top