Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Christopher Chege Msando enzi za uhai wake.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC, Christopher Chege Msando ambaye alitoweka siku ya Ijumaa usiku, amepatikana akiwa amefariki.
Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi majira ya saa 9 alfajiri kupitia ujumbe wa SMS kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake.
“Hakuna shaka kwamba aliteswa na kuuawa,” mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati ameambia wanahabari.
Jeneza lenye mwili wa marehemu.
“Swali pekee lililo katika akili zetu ni kuhusu nani limuua na ni kwa nini aliuawa siku chache hivi kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika,” shirika la habari la AFP limemnukuu Bw. Chebukati akisema.
Polisi wanasema kuwa mwili wa afisa huyo pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la Kikuyu, Kaunti ya Kiambu jijini Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City Mortuary.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top