Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mwanamitindo Jokate Mwegelo.
MWANAMITINDO Jokate Mwegelo amefunguka kuwa pamoja na kukutana na wanamuziki mashuhuri, Shawn Carter ‘Jay Z’, Beyonce Knowles na mchezaji Thiery Henry, mwingine anayetamani kukutana naye maishani ni mwanamuziki Robyn Fenty ‘Rihanna’ pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama na mkewe, Michelle.
Mwanamuziki Rihanna.
Jokate alifunguka hayo juzikati baada kutimiza ndoto yake ya kukutana na mwanamuziki nguli Afrika, Oliver Mtukudzi nchini Afrika Kusini hivyo kuweka wazi kuwa kiu yake imebaki zaidi kwa Rihanna.
“Natamani sana kukutana na mwanamuziki Rihanna pia Obama na mkewe. Rihanna namuelewa sana kwa sababu tunafanana hadi mauombo yetu, itakuwa safi sana nikikutana naye,”alisema Jokate.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top