Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mke wa mwanamuziki Roma ambaye anajulikana kwa jina la Nancy, leo ameamua kufunguka juu ya tukio la kutekwa mumewe, baada ya kupita muda mrefu bila kuzungumzia chochote.
Nancy amefunguka mengi ikiwemo jinsi alivyokabiliana nalo tukio hilo, na jinsi alivyokuwa akiumia baada ya mumewe kugundulika kuwa ametekwa.
Nancy amesema kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza zaidi ni pale mtoto wake alipokuwa akimuulizia baba yake na hajui aliko na kama yupo salama au la, na pia kitendo cha watu kusema tukio la Roma kutekwa lilikuwa ni maigizo, wakati amerudi akiwa na majeraha.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top