Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza maswali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, wakati alipotembelea Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mji mwema, Wilaya ni Kigamboni kukagua maendeleo ya ujenzi huo.Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Gilles Muroto na anayefuatia ni Mkuu wa Utawala Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Benadict Kitalika.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa,akimuonyesha eneo linapotakiwa kujengwa kituo cha Polisi Kibada, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani yaNchi, Mhandisi Hamad Masauni,wakati wa ziara ya naibu waziri,wilaya ni Kigamboni, Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akikagua moja ya chumba cha mahabusu ndani ya kituo cha Polisi Mwasonga, wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya polisi wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Muonekano wa nje wa Kituo cha Polisi cha Mwasonga kilichopo wilayani Kisarawe, kikiwa katika hatua za mwisho kabla ya ujenzi wake kukamilika. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na madereva bodaboda wakati wa ziara ya kikazi wilayani Kigamboni ambapo aliwaasa madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani pindi wafanyapo shughuli zao ili kuepuka ajali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Muendesha Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Said Athumani, akimuuliza maswali Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri huyo wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Muendesha Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Fredrick Swai, akimuuliza swali Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri huyo wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top