Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Bondia,Wladimir Klitschko ametangaza kustaafu katika tasnia ya mchezo wa ngumi mapema leo asubuhi wakati ambapo dunia ikiwa na shahuku kubwa ya kushuhudia pambano la marudiano dhidi ya bingwa wa dunia wa uzito wa juu Anthony Joshua.
Bondia,Wladimir Klitschko akiwa ameanguka chini baada ya kipigo kutoka kwa Anthony Joshua
Klitschko mwenye umri wa miaka 41, amedumu katika mchezo wa ngumi kwa takribani miaka 21 na hivyo kumfanya kuwa mwanamasumbwi pekee aliye dumu kwa muda mrefu, raia huyo wa Ukrain ametumia siku 4,383 katika ulingo akiwania mataji mbalimbali.
Bondia,Wladimir Klitschko (kushoto) akiwa na Anthony Joshua (kulia)
Bingwa huyo wa mchezo wa ngumi amesema imemchukuwa wiki kadhaa kufikiria maamuzi yake ya kustaafu kabla ya kutangaza.
“Nimetumia wiki kadhaa kufikiria maamuzi yangu ya kustaafu ilikupata muda wa kutosha kabla ya pambano la Wembley”
“Nimeshinda kilakitu katika miaka hii 21 niliyotumikia mchezo wa ngumi na ndotozangu zote zimetimia nahitaji sasa kutumia nafasi nyingine nje ya ngumi”.
“Sikiwahi kufikiria kama ningetumia mudamrefu katika tasnia hii na kupata mafanikio makubwa kama niliyonayo kupitia mchezo huu nashukuru kwa hili”.
“Nashukuru kwa kilamtu ambaye amenipa ushirikiano, hususani familia yangu, timu yangu na mashabiki wangu”.
Kutangaza kustaafu kwa Klitschko kuatoa faida kwa Anthony Joshua ambaye alikuwa akijiandaa kwa mchezo wa marudiano wa kutetea ubingwa dhidi ya bondia huyo.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top