Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Jokate Mwegelo na Yvonne Chakachaka.
UKARIBU uliojitokeza hivi karibuni kati ya mwanamitindo, Jokate Mwegelo na mkongwe wa muziki kutoka Afrika Kusini, Yvonne Chakachaka umeibua maswali mengi huku wengi wakihoji kulikoni.Kwa mujibu wa chanzo, Jokate ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa shughuli binafsi, amekuwa akionekana mara kwa mara kuwa karibu na Chakachaka na kufikia hatua ya kufurahia kukutana na mama aliyekuwa akimtafuta kwa muda mrefu.Jojo (Jokate) ana furaha sana kukutana na Chakachaka na muda wote amekuwa akimuita mama… mama, si unakumbuka mwanzoni Ali Kiba naye alishawahi kukutana na Chakachaka wakarekodi na wimbo kisha akaandika katika kurasa zake katika mitandao ya kijamii kwamba anamshukuru mama (Yvonne) kwa kila kitu anachomfanyia.
Alikiba na Yvonne Chakachaka.
“Huenda Jokate anajiweka karibu na Chakachaka kwa sababu ya kuwaonesha watu kuwa yeye na Ali Kiba bado wapenzi na mama yao ndiyo huyu,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Pili kuna picha ambayo Jokate anaonekana akiwa karibu na mtoto wa kiume wa Chakachaka, tena wakiwa katika pozi la mtu na mpenziwe, huenda nalo likawa swali lingine lisilo na majibu, si unamjua Jokate ni mtu wa kimyakimya.”
Jokate Mwegelo na Yvonne Chakachaka.
Baada ya kupata ubuyu huo, Ijumaa lilimtafuta Jokate kwa njia ya WhatsApp na kumbana kuhusiana na ishu hiyo ambapo alipopatikana alifunguka;
“Jamani hakuna chochote kinachoendelea zaidi ya kuwa na Yvonne (Chakachaka) kwenye projekti ya kijamii ya wanawake na watoto. Namshukuru Mungu kwani amenikutanisha na mtu ninayempenda na anayenipenda mimi na kazi zangu, hivyo nitaendelea kuwa karibu naye na si kwa vingine kama watu wanavyofikiria.”

STORI: IMELDA MTEMA, DAR


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top