Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mratibu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo Pichani) kuhusiana na mchezo wa bahati nasibu ya Tatu Mzuka, wakati wa uzinduzi wa mchezo huo wa kubahatisha nchini mapema jijini Dar es salaam (picha na ImmaMatukio Blog)

Na Mwandishi Wetu

Tatu Mzuka ni mchezo mpya wa jackpot uliobuniwa mahsusi kubadilisha maisha ya watu. Tatu Mzuka ni rahisi kucheza kwa kutumia simu ya mkononi, na kushinda ni baada ya kila lisaa limoja baada ya kucheza.

Kucheza Tatu Mzuka unahitaji kuchagua namba zako tatu za bahati, kati ya 0 na 9 kwa kufanya muhamala kwenye simu ya mkononi, linganisha namba mbili ili kujiongezea nafasi ya kushinda mara mbili, au linganisha namba tatu na ushinde mara 200. 

Akieleza sababu ya kutumia namba tatu, Mratibu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga alisema, “tumezungukwa na namba,, inaweza kuwa siku yako ya kuzaliwa, namba ya jezi ya mchezaji unayempenda au kumbukumbu yoyote hivyo tunaamini kila mtu anazo namba angalau tatu za bahati, sasa fikiria kutumia namba yako ya bahati kujishindia mamilioni ya fedha.”

Balozi wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein akitambulisha Tatu mzuka kwa waandishi wa habari

Unaweza kubeti kuanzania Tsh 500 mpaka Tzsh 30,000 na kujiwekea
nafasi ya kushinda mpaka Tzsh milioni 6 ndani ya lisaa. Kubeti na Tatu
Mzuka ni kupitia huduma za fedha kwa njia ya mtandao, hivyo hutahitaji
kufanya usajili wowote. Fedha utakazoshinda pia zitatumwa moja kwa moja
kwenye simu yako.

“Kila unapobeti unaingia moja kwa
moja kwenye droo ya wiki iitwayo Mzuka Jackpot, na droo hii inakupa
nafasi ya kuwa milionea, hivyo basi kwa kila Tzsh 500 unayobeti kwenye
Tatu Mzuka, unapata nafasi moja ya kuingia kwenye droo ya Mzuka
Jackpot,” alieleza Maganga.

Aliongeza kuwa, kila
ticket ya Tatu Mzuka inakuwa na viashiria vyenye herefu 6 zanazokuingiza
kwenye droo ya Jackpot, hivyo ukibeti Tzsh 500, herufi zako zinaingizwa
kwenye droo mara tatu, hivyo kukuongezea nafasi ya kushinda.

Muwakilishi
kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Daniel Wilson amewasihi
watanzania kushiriki kwenye Tatu Mzuka na kuwa na nafasi ya kubadilisha
na kuboresha maisha yako. Sera ya Tatu Mzuka ni uwazi, hivyo kila
ushindi wa washiriki utachapishwa kwenye tovuti ya Tatu Mzuka (www.tatumzuka.co.tz).

Droo
ya Jackpot itafanyika kila Jumapili na kurushwa moja kwa moja na vituo
vya televisheni vya TV1 na Clouds TV saa 3 kamili usiku na kutangazwa na
mtanganzaji mashuhuri Mussa Hussein akiambatana na Antu Mandoza. Kila
mshindi atakua na uhakika wa kushinda kati ya Tzsh milioni 2 na milioni
6, pamoja na kupata nafasi ya kujishindia milioni 30. Iwapo hakuna
atakayeshinda milioni 30, basi wiki inayofata, kitita cha Mzuka Jackpot
kitaongezeka mara mbili yake na kuwa milioni 60.

Ndani
ya wiki moja tu tangu kuanza kwa Tatu Mzuka, wameshapatikana washindi
zaidi ya 40,000, na kulipwa kiasi cha Tzsh milioni 100 kwa pamoja. Beti
na Tatu Mzuka sasa upate nafasi ya kushinda Tzsh milioni 60 Jumapili
hii.

Mmoja wa waandishi wa habari akishiriki katika droo ya Tatu Mzuka wakati wa uzinduzi

Balozi wa Tatu Mzuka, Shilole akishiriki katika mchezo huo wa kubahatisha mapema leo

Baadhi ya Waandishi wa Habari waliokuwepo katika shughuli ya uzinduzi wa mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka mapema leo katika hoteli ya Serena
Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top