Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii Juma Nature amewakingia kifua wasanii wa kike wa zamani ambao Gigy Money amesema walikuwa hakuna cha maana wanachokiimba, na kumtaka atulie kwani bado ni mdogo kwenye tasnia.
Juma Nature amesema kitu ambacho Gigy Money anatakiwa kufanya sasa hivi ni mazoezi ili aweze kuandika nyimbo, na sio kuongea hovyo kuponda watu wazima, kwani hajapitia mikiki kwenye maisha ya muziki.
"Hawezi kuwa na dharau wakati mtu mwenyewe hata albam saba hajafikisha, bado mdogo sana afanye mazoezi atunge nyimbo zenye hekima, anaweza akapata matuzo kibao, lakini asiongee ongee hovyo bado mdogo sana huyo mtoto, hajawahi kupata mikiki, aingie kwenye mikiki mikiki awaulize wenzake kina Zay B  watamfundisha wanawake wenzake, sisi wanaume kwetu ndiyo asiingie kabisa kwa sababu huku vitani", alisema Juma Nature.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top