Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho.
NAHODHA wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard, amemweleza kiungo wa timu hiyo Philippe Coutinho, kama anataka vita basi alamishe kwenda Barcelona.
Barcelona wameshapeleka ofa mara mbili wakimtaka kiungo huyo raia wa Brazil wakiwa na presha kubwa baada ya Neymar kuondoka hapo na kujiunga na PSG.
Nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard.
Barca wameshaweka wazi kuwa mchezaji anayeweza kuziba pengo la Neymar ni Coutinho tu, hivyo wamekuwa wakipambana sana kuhakikisha wanampata.
“Ni vigumu kumzuia asiondoke, sana sana wachezaji wanaotoka Amerika ya Kusini ambao mara nyingi wamekuwa wakisema kuwa ni ndoto yao kucheza Barcelona.
“Lakini nafikiri Barca wameleta ofa mbili nazo zimekataliwa, nafikiri kama akilazimisha kwenda atakuwa anategeneza vita kwa kuwa Liverpool hawawezi kumuachia kwa urahisi,” alisema Gerrard.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top