Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Kijana Adam Mwangoka akiugulia baada ya upasuaji.
AMA kweli hujafa hujaumbika! Kijana Adam Mwangoka (21), mkazi wa Arusha, amepatwa na gonjwa la ajabu la macho yake kuvimba na kutoka kwa nje kama yanataka kudondoka, hali iliyomsababishia ateseke na kushindwa kutimiza majukumu yake kama zamani.
Akizungumza na Gazeti la Amani, dada wa Adam, Salma Mwangoka kuhusu tatizo la mdogo wake alisema: “Nilikuwa naishi na mdogo wangu tangu alipomaliza darasa la saba, niliamua kukaa naye baada ya kushindwa kuendelea na masomo ya sekondari.
Akifanyiwa matibabu.
“Kwa kuwa alikuwa anapenda ufundi wa magari nilimsaidia akajifunza umakenika hadi akaelewa na baadaye aliniaga kuwa kuna gereji amepata iko jijini Mbeya hivyo anaomba ruhusa ili aende akafanye kazi kule. Nilifurahi kwa hatua ile nikamtafutia nauli.
“Ilipofika mwezi Julai, mwaka jana akanipigia simu kuwa macho yake yanatoa machozi sana na amefikia hatua hawezi kufanya kazi kwa sababu ya macho kumsumbua.
“Baadaye akaanza kuumwa kichwa, miguu ikawa inawaka moto. Nilimtumia hela aende hospitalini lakini baadaye akaniambia ameshauriwa aende hospitali kubwa kutokana na tatizo lake.
Matibabu yakiendelea.
“Tangu hapo akawa anaumwa, mara magoti yanavimba, akawa hawezi kabisa kwenda kazini, nikamtumia nauli arudi nyumbani.Sikuamini siku niliyompokea mdogo wangu, macho yalikuwa yametoka nje sana ingawa kwa sasa tatizo lake limeongezeka zaidi. Ilipofika Machi, mwaka huu ndiyo yakapasuka na kuwa kama yanataka kudondoka. Naumia sana mdogo wangu anavyoteseka, nilimpeleka Hospitali ya KCMC lakini hali yake bado haijawa sawa.
Hali yake ilivyo.
UWEZEKANO WA KUONA UPO
“Kwa mujibu wa madaktari uwezekano wa kuweza kuona upo, kikubwa ni pesa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji, mimi mwenyewe
sina pesa kwani hata kumpeleka K.C.M.C nilichangiwa pesa na wanakijiji.
Akiugulia kitandani.
MGONJWA AKATA TAMAA
“Hivi karibuni mdogo wangu aliniumiza sana baada ya kusema kuwa nimrudishe nyumbani kwani anaona kama anateseka tu na hawezi kupona.
KWA ALIYEGUSWA NA TATIZO LA KIJANA HUYU
Kwa mtu yeyote aliyeguswa na tatizo la kijana huyu, anaweza kumsaidia chochote ili kukamilisha matibabu yake. Wasiliana naye kwa namba 0759118647, imesajiliwa kwa jina la Evaline Mruma.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top