Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Kikosi cha Simba.
STRAIKA mpya wa Simba, John Bocco amewapiga biti wapinzani wa kikosi hicho kwa kuwaambia wakae chonjo na kujiandaa kuikabili safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho ambayo inaongozwa na utatu unaoundwa na yeye, Shiza Kichuya pamoja na Mganda, Emmanuel Okwi.
Kwa mara ya kwanza utatu huo wa Bocco, Kichuya na Okwi ulicheza kwa pamoja kwenye mchezo wa siku ya Simba, Simba Day, dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, ambapo wachezaji hao walionyesha uwezo mkubwa na kuisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Okwi akishangilia bao na Mohamed Ibrahim pamoja na Kichuya.
“Kila mmoja ameona jinsi ambavyo tulivyocheza kwenye mechi ya Simba Day, lakini pale ni mwanzo tu lakini bado tuna kazi kubwa ya kuifanyia timu hii, hasa sisi washambuliaji ambao ndiyo tunabeba jukumu kubwa la kufunga mabao.
Bocco akifanya yake.
“Naamini kwa kupitia utatu wetu ambao tunauunda wa mimi, Kichuya na Okwi kuna kitu ambacho tutakuja kukifanya, labda niwape neno wapinzani wetu ni lazima waanze mipango thabiti ya kuhakikisha wanatuzuia kwani tutakuja na moto mkubwa kuliko wa mechi hii,” alisema mshambuliaji huyo ambaye ni nahodha msaidizi wa timu hiyo.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top