Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Zitto Kabwe.
KIONGOZI Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, katika kile kilichoonekana kuwapa kijembe Chadema, akisema kutaka nchi kunyimwa misaada ni uhayawani, kwani vita dhidi ya kuminywa kwa demokrasia inapaswa kupiganwa ndani.
Zitto alitoa kauli hiyo kupitia akaunti yake katika Mtandao wa Kijamii wa Twitter, ikiwa ni siku moja tu baada ya Chadema kupitia kwa mwanasheria wake, Tundu Lissu kuitaka Jumuia ya Kimataifa kuinyima Tanzania misaada kufuatia kitendo cha kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa viongozi wa upinzani, hasa kutoka chama chao.
“Huu ni uhayawani, hii ni nchi huru, kukaribisha wageni kuingilia mambo yetu ni upuuzi na umazwazwa, tupambane ndani kuleta demokrasia,” aliandika Zitto.
Hata hivyo, kufuatia kauli hiyo baadhi ya watumiaji wa mtandao huo walianza kumuuliza maswali kadha Zitto ambaye aliwajibu na kuufanya mjadala huo kuwa mrefu, baadhi wakimuunga mkono na wengine wakipingana naye.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top