Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail ThisMAHAKAMANI KISUTU: Mfanyabiashara Yeriko Nyerere anayekabiliwa na kesi ya uchochezi wa kimtandao, mapema leo Julai 6 amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuti, Dar kusikiliza kesi yake hiyo ambayo hata hivyo imeahirishwa hadi Agosti 7 mwaka huu.


Kesi hiyo imeahirishwa na Hakimu Willibard Mashauri kutokana na hakimu anayeisikiliza kesi hiyo, Godfrey Mwambapa kutokuwepo mahakamani hapo.


Yeriko anakabiliwa na mashtaka matano ya kutoa taarifa za upotoshaji kwa njia ya mtandao ambapo kesi hiyo ilitakiwa kusikilizwa ushahidi leo.Katika kesi hiyo mawakili wanaomtetea mshitakiwa ni Tundu Lisu na Peter Kibatala.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top