Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baadhi ya wenye vipara wamekuwa wakiuawa nchini Msumbiji kutokana na imani za kishirikina ambapo inaaminika kufanya hivyo ni kijipatia utajiri wa haraka na wengine kudai vichwa vya watu hao vina dhahabu.
Hadi sasa Polisi katika jimbo la Zambezia nchini Msumbiji wamewakamata watu wa nne kwa kuhusika na mauaji ya watu wenye vipara. Pi wanaendelea na uchunguzi huku wakifuatilia zaidi kujua nani anachochea mauaji hayo.
Waganga wa kienyeji wamekuwa wakidaiwa kusambaza habari zisizo na ukweli kwamba vichwa vya watu wenye vipara vimekuwa na dhahabu.
Pia Polisi wamekuwa wakichunguza mauaji ya albino ambao wamekuwa wakikatwa viongo vyao vya mwili, na kutumika katika masuala ya imani za kishirikina


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top