Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto) akipokelewa na Mwakyembe alipowasili kumpa pole nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kwa msiba wa kufiwa na mkewe.
Wakiongea jambo.
Waziri Mkuu akisalimia waombolezaji kwenye msiba huo.
Familia ya Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Harisson Mwakyembe, imepatwa na msiba mkubwa baada ya kuondokewa na mpendwa wao, Lina Mwakyembe, ambaye ni mke wa waziri huyo.
Lina amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu saratani ya titi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewaongoza waombolezaji na viongozi mbalimbali wa serikali katika msiba huo uliopo Kunduchi, Mtongani, jijini Dar es Salaam, akiwataka wanafamilia kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha msiba.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top