Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maagizo ya kuvunjwa kwa Baraza la Michezo Tanzania(BMT) na kuelekeza shughuli zake kufanywa na Sekretarieti hadi hapo Baraza jipya litakapoundwa tena.
Maagizo hayo yametolewa jana bungeni mjini Dodoma na Mh. Majaliwa wakati akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa saba wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akiongeza kwamba serikali haitavumilia usimamizi mbovu wa michezo. 
“Serikali ya awamu ya tano haitafumbia macho usimamizi mbovu na utawala wa michezo usiojali maslahi ya Taifa, Serikali imeazimia kuimarisha utendaji kwa vyombo vya michezo nchini ili kila mwenye dhamana awajibike ipasavyo,” alisema Mhe.Majaliwa. 
Mbali na hayo Mh. Majaliwa ameipongeza kwa dhati timu ya Serengeti Boys kwa kutoa upinzani mkubwa kwenye mashindano ya shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika na kuweka msisitizo kwa Chama cha Mpira nchini (TFF) kuendelea kuwatunza vijana hao. 
“Msisitizo wangu kwa TFF ni kuendelea kuwatunza vijana hao na kusimamia vilabu vya michezo nchini, kuwekeza kwenye soka la vijana ili kujenga timu imara kwa miaka michache ijayo,” aliongeza Majaliwa.
Kuhusu michezo shuleni Mh. Waziri Mkuu amesema kwamba  “Tutaendelea kuratibu michezo shuleni, ikiwa ni pamoja na kusimamia ufundishaji wa michezo kama somo, kwani serikali inatambua umuhimu wa michezo kwa Afya, inaleta umoja wa kitaifa pia ni fursa ya ajira kwa vijana wetu ambapo ivi karibuni mkoani Mwanza yamehitimishwa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA yaliyoibua vipaji na hamasa kubwa iliyo miongoni mwa vijana nchini.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top