Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DCP, Lucas Mkondya akiwaonyesha wanahabari bangi zilizokamatwa na jeshi hilo.

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limesema kuwa limefanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa 250kwa makosa mbalimbali ya kihalifu yakiwemo ya kukutwa na madawa ya kulevya.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Lucas Mkondya ameeleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kupitia msako mkali kuanzia Julai 16, hadi leo Julai 17 ambapo watuhumiwa hao walikamatwa.

Mkondya amesema, miongoni mwa makosa waliyokamatwa nayo watuhumiwa hao ni pamoja na kupatikana na madaya ya kulevya, unyang’anyi wa kutumia silaha, utapeli na kucheza kamari.

Aliongeza kuwa upelelezi wa makosa hayo ukikamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top