Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Aliyekuwa mke wa Dk. Harrison Mwakyembe, Bi Linah George Mwakyembe, enzi za uhai wake.


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,  Prof Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiongea na Mwakyembe.


Prof Elisante Ole Gabriel akiongea na wanahabari.

Waombolezaji wakiwa msibani.

Waombolezaji wakiendelea kumpa pole Mwakyembe.

Mwombolezaji William Malecela akiongea jambo na Mwakyembe.
Familia ya Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Harisson Mwakyembe, imepatwa na msiba mkubwa baada ya kuondokewa na mpendwa wao, Lina Mwakyembe, ambaye ni mke wa waziri huyo.
Lina amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu saratani ya titi.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Solomon Kivuyo,  marehemu Lina  alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda mrefu karibu  miaka miwili akiwa anatibiwa hospitali mbalimbali duniani.
Pia, alishawahi kulazwa katika hospitali za  Muhimbili,  Aga Khani,  India na Uturuki.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa Kyela, mkoani Mbeya, siku ya Jumatano  ijayo .


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top