Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Kinara wa Matokeo ya Kidato ch Sita 2017 kwa masomo ya Sanaa Kitaifa, Francis Thomas (katikati) wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Feza (Feza Boys).

Sophia Juma, mwanafunzi wa St Marry’s Mazinde Juu ya Tanga (picha yake haijapatikana) ameibuka kidedea katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa leo Jumamosi, Julai 15, akishika namba moja kitaifa.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde imeeleza kuwa nafasi ya pili imeshikwa pia na msichana, Agatha Julius Ninga wa Tabora Girls. Wote walikuwa wakichukua masomo ya mchepuo wa Sayansi (PCB).


Kadhalika taarifa hiyo imeeleza kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).Francis Thomas akiwa na wazazi wake ambao ni Thomas Samky na mama yake Victoria Samky.

Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.
Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385.

Katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Feza (Feza Boys), mwanafunzi Francis Thomas ameibuka kinara wa masomo ya Sanaa (Arts) Kitaifa wakati Feza Girls, wanafunzi Atuganile Jimmy ameshika nafasi ya nane Kitaifa na wa tatu kwa wasichana huku Kabhabhela Bukuru wa shule hiyo akishika nafasi ya Saba kwa wasichana Kitaifa.

FEZA GIRLS YAONGOZA MATOKEO KIDATO CHA SITA

“Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la 1-11  umepanda  kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;
“Pia ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana.”


Francis akibebwa na wanafunzi wenzake wa Feza Boys,.

Shule zilizoongoza
Katika matokeo hayo, Shule ya Wasichana ya Feza Girls ya Dar es Salaam imeibuka kinara kwa watahiniwa wake 67 kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili.
Shule nyingine zilizoibuka kidedea katika matokeo hayo ni Marian Boys (Pwani) iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika nafasi ya tatu na Ahmes (Pwani) imeshika nafasi ya nne.
Shule nyingine  ni  Marian  Girls (Pwani) iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe (Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba, Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza Boys (Dar es Salaam) nafasi ya tisa na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi.


Wanafunzi wa Feza Girls ambayo imekuwa ya kwanza Kitaifa, kushoto ni Atuganile Jimmy aliyeshika nafasi ya nane Kitaifa na wa tatu kwa wasichana akiwa na Kabhabhela Bukuru ambaye amekuwa wa Saba kwa wasichana Kitaifa.

Shule zilizoshika mkia
Shule zilizoshika mkia ni Kiembesamaki ya Unguja, Hagafilo (Njombe), Chasasa (Pemba), Mwenyeheri Anuarite (Dar es Salaam) na Ben Bella (Unguja). Nyingine zilizotajwa kushika mkia ni Meta (Mbeya) na Mlima Mbeya (Mbeya).
Nyingine ni Shule ya Sekondari ya Al-Ihsan Girls (Unguja) na St Vicent(Tabora).

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YATANGAZWA, BOFYA HAPA KUYAONA

Waliofutiwa matokeo
Kadhalika taarifa ya Necta imeeleza kuwa watahiniwa 10 walifutiwa matokeo kwa makosa ya kufanya udanganyifu.
Taarifa ya Dk Msonde imeeleza kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea.

NECTA YAWAFUTIA MATOKEO WANAFUNZI 10 WA KIDATO CHA SITA

Pamoja na hao kumi, watahiniwa wengine 15 hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo kutokana na  matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa kufanya mitihani hiyo.
‘Watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018 kama watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde.
Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018.


TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI TANZANIA (NECTA)

MATOKEO KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2017

MATOKEO YA DIPLOMA YA UALIMU (DSEE) 2017

MATOKEO YA CHETI CHA UALIMU (GATCE) 2017Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top