Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Maleu Mrema.
Mfanyabiashara maarufu nchini, Maleu Mrema amefariki dunia jana akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.
Ndugu wa marehemu,Vincent Laswai alithibitisha msiba huo akiwa nyumbani kwa marehemu eneo la Uzunguni jijini Arusha.
Akihojiwa na gazeti hili Laswai amesema kwamba alipokea taarifa za kifo cha marehemu jana saa 12 jioni na uongozi wa familia utatoa taarifa za kifo cha mfanyabiashara huyo leo.

Hoteli ya Impala.
Laswai, amesema kwamba ni mapema kuzungumzia chanzo cha kifo kwa sababu bado hawajapata taarifa kutoka katika hospitali aliyokuwa akitibiwa nchini humo.
Hivi karibuni marehemu Mrema alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya ambapo Juni mwaka huu alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.
Mrema alikuwa akimiliki Hoteli za Ngurdoto, Impala na Naura Springs za jijini Arusha.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top