Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imetupwa nje ya michuano ya COSAFA baada ya kipigo cha goli 4-2 kutoka kwa timu ya taifa yaZambia maarufu kama Chipolopolo.
Stars ilianza kupata bao kupitia Erasto Nyoni lakini Zambia wakasawazisha na kuongeza na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1.

Baada ya Nyoni kuumia na kutolewa, mabeki wa kati Salim Mponde na Abdi Banda wakaonekana kuyumba na kutoa nafasi kwa Washambuliaji wa Zambia kuongeza mashambulizi

Kipindi cha pili, Zambia walipata mabao mawili ya haraka na kuwa 4-1 lakini Simon Msuva alifunga bao lingine la kufuta machozi na matokeo ya mpaka dakika ya 90 4-2.

Hata hivyo Taifa Stars kwa matokeo hayo itasubiri mshindi wa mechi ya baadae kati ya Lesotho na Zimbabwe na kucheza nae Ijumaa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo ya COSAFA.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top