Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mrembo kutoka tasnia ya filamu nchini, Wema Sepetu ameonekana kukerwa na kitendo cha baadhi ya wanawake kupenda kupiga picha za utupu kuonyesha matumbo yao wakati wa ujauzito.

Utakumbuka miezi miwili iliyopita muimbaji wa Bongo Flava, Linah aliteka vichwa vya habari kwa kuachia picha za nusu utupu za ujauzito wake, pia baby mama wa Diamond Platnumz, Zari aliwahi kufanya hivyo kipindi cha ujauzito wa mwanae Tiffah. Hiyo ni kwa upande wa watu maarufu.
Sasa Wema Sepetu katika ukurasa wake wa Instagram ameandika, “Mashallah Esha wangu… Staha hadi Raha…. Sijawahi Elewa Wanawake wakishaenda kwenye Maternity shoots kwanini wanataka sana wakae uchi…. This Is Very Beautiful my Darling…. Allah Bariq Tumbo lako ujifungue salama my love… Unajua navyokupenda…. Hii iende kwa wanaokaaga Uchi wakiwa wanapiga picha za Mimba Jamani@esha.s.buheti @esha.s.buheti”
Katika kujibu comment mbali mbali za mashabiki wake katika mtandao huo aliongeza, “…… Mi sijawahi elewa maana kwanza Tumbo linakuaga na ule mstari jamani…. Ifind it very private… Ila kila mtu ana maamuzi yake mwanangu…. Inshallah Allah akanijalia kufika hapa, KATU siwezi muonesha mdogo wako ovyo…. Kwanza unichape nikifanya huo upuuzi


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top