Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


“Mimi naomba umesomea IT kaibe Bank, umesomea IT kafungue ndege sio unakuja kuhack akaunti za wasanii mnatuyumbisha!!!. Halafu mnasema tunawapenda wasanii wetu, sio kweli,” hayo ni maneno ya Shilole kwa wale waliodukua akaunti yake Instagram.
Muimbaji huyo wa Bongo Flava siku kadhaa zilizopita aliripoti kudukuliwa kwa akaunti hiyo ambayo alikuja kufanikisha kuirejesha, hata hivyo ameapa kula sahani moja na waliofanya hivyo.
“Kiukweli wanatuharibia sana, ukiangalia mimi Instagram yangu inanisaidia kutangaza muziki wangu katika jamii. Unapoenda kuhack akauti yangu huna faida nayo, unanikwamisha. Kama mmesoma IT simkaharibu maeneo makubwa, mkaibe Bank mpate pesa, ukija kwenye akauti yangu hapati chochote, so waache haisaidii kitu chochote, yaani haida faida,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.
“Nikimfahamu mtu aliyefanya ninataka afungwe na iwe fundisho kwa wengine na mimi bado nipo nae nanitamjua, yaani lazima hata kama nitamuendea kwa mganga wa kienyeji,” amesisitiza Shilole.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top