Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford.
WAKATI ndoa yake na Rashid Said ‘Chid Mapenzi’ ikiwa na miezi kumi bila kujibu kwa kupata ujauzito, staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ameibuka na kufunguka sababu iliyomfanya kutobeba mimba hadi sasa.

 Shamsa Ford akiwa na mapenzi wake Rashid Said ‘Chid Mapenzi’ (kushoto).
Shamsa aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, watu wengi walishakariri kwamba mtu akiingia kwenye ndoa tu, anapata ujauzito kwa kipindi kifupi, jambo ambalo kwa upande wake ni tofauti kwa kuwa yeye na Chid Mapenziwalikubaliana kujipanga kimaisha kwanza ndipo waanze kutafuta mtoto. “Tunajipanga kwanza kimaisha.
Hatuwezi kukurupuka tu ila ndani ya mwaka huu tunaanza kutafuta mtoto na tunamuomba Mungu atusaidie maana mtoto hutoka kwa Mungu, siyo kwa binadamu na kwa kuwa tutakuwa tumeshajipanga watakuwa wanapishana miezi sitasita tu,” alisema Shamsa mwenye mtoto mmoja aliyezaa na jamaa aitwaye Dickson Matoke.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top