Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’

IMEVUJA! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, anatajwa kuwa ndiye staa pekee wa kike Bongo aliyeweka rekodi katika utawala wa Serikali ya Rais Dk.John Pombe Magufuli ‘JPM’ baada ya hivi karibuni kumfanyia kufuru ya fedha msanii mwenzake, Muhsein Awadh ‘Dk. Cheni’.

Chanzo kilichokuwa eneo la tukio kililieleza Risasi Jumamosi kuwa, Lulu alifanya kufuru hiyo miezi kadhaa iliyopita katika harusi ya shemeji wa Dk. Cheni iliyofanyika Msasani Tower jijini Dar ambapo Lulu alimtuza Dk. Cheni fedha nyingi, yaani noti za elfu kumikumi zisizo na idadi hali iliyomsababisha jamaa huyo na mkewe kushindwa kuzishika mikononi na kuziweka kwenye bahasha kubwa ya kaki.


Dk. Cheni

“Pamoja na Magufuli kukaba kila kona na mastaa wenzake kufulia, lakini Lizy (Lulu) ana jeuri kama kawa. “Kiukweli kwa fedha alizommwagia Dk. Cheni, inaonekana yupo vizuri sana kifedha kuliko wasanii wengine maana siyo kwa kufuru aliyomfanyia Dk. Cheni mpaka wageni waalikwa wakabaki wamepigwa na butwaa. Watu walibaki wakijiuliza anapata wapi fedha kiasi hicho ukizingatia hali ya maisha ni ngumu sana katika utawala huu wa JPM,” kilidai chanzo.

Baada ya kupata ubuyu huo na kunasa video inayomuonesha Lulu akimtuza minoti mingi Dk. Cheni na mkewe, Risasi Jumamosi lilimtafuta Dk. Cheni ili kumsikia kauli yake kwamba alijisikiaje ambapo alisema alijisikia furaha sana.

“Ile ilikuwa ni harusi ya shemeji yangu ambayo ilifanyika pale Msasani Tower, kwa kweli nilifurahi sana Lulu kututuza mahela yale maana mtu ukipewa zawadi siku zote lazima ufurahi,” alisema Dk. Cheni.

Uchunguzi wa Risasi Jumamosi ulionesha kuwa, Lulu, tofauti na wasanii wengine wanaolia maisha magumu, amekuwa akifurukuta kwenye utawala huu kwa kufanya kufuru kwani licha ya kuonekana akimtuza Dk. Chenipia amekuwa akipigilia pamba za gharama kiasi cha kuwafanya watu kuhoji, anazichota wapi pesa za kufanyia kufuru?


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top