Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baada ya kutupiwa virago na mpenzi wake wa zamani, diva kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Jacqueline Wolper, amempata ‘baby’ mwingine ambaye kuthibitisha kuwa amefika, amejichora tattoo yenye jina la staa huyo.

Mpenziwe huyo, mwanamitindo anayefahamika kwa jina moja la Brown amejichora tattoo hiyo ikiandikwa Nakupenda Wolper na mara moja mrembo huyo ameitupia katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram bila kusema lolote huku maneno hayo yakionekana wazi


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top