Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail ThisMUUZA nyago machachari Bongo, Gift Stanford `Gigy Money’, anadaiwa kuwekwa kinyumba na mtoto wa kigogo maeneo ya Masaki jijini Dar, baada ya kumwagana na aliyekuwa mwandani wake, Mourad Alpha ambaye ni mtangazaji wa Choice FM.

Kwa mujibu wa chanzo kilichopo karibu na Gigy, mwanadada huyo amekolea kwenye penzi la mtoto huyo kiasi cha kuikimbia nyumba aliyokuwa akiishi Mbezi-Beach, Dar na kwenda kuishi Masaki kwa jamaa huyo ambaye sasa wanapika na kupakua.

Baada ya kuunyaka ubuyu huo, paparazi wetu alimtafuta Gigy ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa akijiita Gigy wa Masaki ambapo alicheka na kusema: “Nilipopataka nimepapata, huyu ndiye mwanaume wa hadhi yangu ila sipo tayari kumuanika kwa sasa.”


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top