Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baraka The Prince amefunguka na kutaja list ya wasanii wa Rnb anaowakubali kutoka Tanzania na kusema wapo wasanii wengi wa muziki huo ambao wanafanya vizuri na yeye kupenda kazi zao lakini wapo wachache ambao anawakubali zaidi kutokana na uwezo wao.
Baraka The Prince amewataja wasanii hao kuwa ni pamoja na Ben Pol, Rama Dee, Barnaba Classic , Bele 9 pamoja na yeye mwenyewe kuwa ndiyo mafundi wa muziki wa Rnb Tanzania 
"Mtu kama Belle 9 unaweza kuona ni mbaya sana angalia chorus zake katika ngoma mbalimbali jinsi anavyoua, Barnaba Classic pia anafanya Rnb nzuri japo kuna wakati mwingine yeye anatumia 'beat' ambazo si za Rnb ila muimbaji mzuri sana, yupo Ben Pol napenda kazi zake lakini brother Rama Dee pia anafanya vyema sana" alisisitiza Baraka The Prince 
Mbali na hilo Baraka The Prince anasema ukimya wake kwenye muziki kwa miezi kadhaa hii utaleta mshangao kwa mashabiki zake pindi atakapoanza kuachia kazi alizozifanya kipindi yupo kimya, pia amedai album yake imekamilika na muda wowote inaweza kutoka mambo yakikaa sawa.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top