Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii Alikiba ambaye sasa yupo nchini Afrika Kusini amewataka mashabiki zake kumuombea kwani yupo kwenye vita vikali, hivyo maombi ndiyo kitu pekee kinachoweza kumfanya kushinda na kuendelea kuwapa burudani wanayotaka.
Alikiba alisema hayo jana baada ya kusaini mkataba na RockStar na kuingia ubia wa kibiashara na kampuni hiyo ambapo sasa naye anakuwa mmoja kati ya wamiliki wa kampuni hiyo.
"Mashabiki zangu nahitaji sana dua zenu, mniombee tu kwani vita ni vingi sana lakini kikubwa niombeeni, nimefurahi kuungana na Rockstar kama mmiliki na tuna malengo makubwa, napenda kuona wasanii ambao wapo chini ya Rockstar wanafanikiwa kama ambavyo mimi nimefanikiwa, na muda si mrefu tutatangaza wasanii wengine waliopo chini ya Rockstar" alisema Alikiba 
Mbali na hilo Alikiba alitangaza ujio wake mpya ndani ya siku chache zijazo na kudai sasa ataachia wimbo wa peke yake kwanza kabla ya kuanza kuachia collabo zake ambazo zipo ndani.
"Collabo zipo ndani ila sasa nitaachia kazi ya pekee yangu maana sijatoa wimbo wa peke yangu kwa muda mrefu, kwa hiyo naleta msiba muda si mrefu kutoka leo kwani kila kitu kipo tayari, hivyo mashabiki kilio chenu kimesikika ".alisisitiza Alikiba 
Alikiba toka ameachia kazi yake ya mwisho 'Aje' ni mwaka mmoja na miezi miwili imeshapita


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top