Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Kipindi cha nyuma kulikuwa na taarifa za Alikiba kufanya kolabo na Yvonne Chaka Chaka na Davido lakini hadi leo hazijatoka, sasa Alikiba amelizungumzia hilo.
Muimbaji huyo wa Bongo Fleva ambaye December mwaka jana alionekana akiwa studio nchini Afrika Kusini na Yvonne Chaka Chaka, kuwa kazi na Mwana Mama huyo ilishafanyika ila kuna mipango inaweka sawa kwanza.
“Kiufupi kwamba nyimbo zipo na taratibu tulishafanya kama mlivyoona tupo studio lakini kuna ratiba lazima ziwepo sio tu umefanya halafu unatoa. Kuna mipango tupo nayo tayari na kila nyimbo itatoka kwa muda wake, na wimbo wangu unatoka hivi karibuni siwezi nikasema ni lini,” amesema Alikiba.
Kuhusu kolabo na Davido alisema, “unajua wasanii kama wasanii muda mwingine tunakuwa na maneno ya kuridhisha watu lakini kiukweli hakijafanyika chochote ila plan zipo za kufanya na muda tukiupata tutafanya il sijajua ni lini kwa sabau nyimbo nilizonazo ni nyingi sana,” amesisitiza.
Mwaka 2015 Davido aliwahi kuulizwa kuhusu na kolabo na Alikiba na jibu lake lilikuwa, “I have a song coming out with Alikiba too, that’s gonna be crazy”.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top