Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa hip hop Bongo, Young Killer ametaja vigezo vitatu iwapo unataka kumsaini katika record label.
Rapper huyo ametaja vigezo hivyo kuwa ni uwezo mkubwa wa kufanya kazi, fedha na connection za mambo ambayo yatajenga muziki wake.
“Sio lazima iwe kubwa ila iwe na uwezo wa kufanya kazi katika kiwango kikubwa, pia ni lazima iwe na hela kwa sababu now day muziki umekuwa biashara na unahitaji hela. Mimi nimekuwa nikifanya kazi mwenyewe lakini nimekua nikipigania sana kile kidogo ninachokipata na kuweza kikiwekeza katika muziki wangu,” ameiambia Radio One na kuongeza.
“Kitu kingine kikubwa lazima iwe na connection sio lazima iwe kubwa lakini iwe na baadhi ya connection angalau hata wawe wanajua wapi tunaanzia na tunapomalizia, kwa hiyo nafikiri naweza kuwa chini ya label hiyo endapo itakuwepo au kupatikana,” amesisitiza.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top