Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Young Killer amedai anaamini katika beef kwani ni kitu ambacho kinachangamsha game.
Katika kukoleza kauli yake rapper huyo ameeleza kuwa nchini Marekani kuna wasanii wengi wamefanya vizuri lakini hawazungumziwi kama Tupa na B.I.G ambao walikuwa na beef.
“Tupac na B.I.G watu mpaka leo wanaendelea kuwaongelea kwa sababu walikuwa hawapatani, walikuwa washikaji baadae wakavunja ushikaji wakawa maadaui, ule uadai wao umefanya hadi biashara yao imekua kubwa na itaongelewa miaka yote,” ameiambia E-Newz ya EATV.
Hata hivyo Young Killer amesema hapendi kuwa na beef na msanii yeyote ila anachojaribu kufanya ni kuwachana baadhi na kuwaeleza ukweli, na ujasiri huo anaupata kutokana hana ushikaji na wasanii.
“Watu wanaogopana sana, mchane akijibu tunachangamsha game inazidi kusogea, now day ukiangali game hata imeanza kuchangamka, unaona Nay amenichana, nimemjibu na imechangamsha,” amesema Young Killer.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top