Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Stamina amefunguka kwa kutoka maoni yake iwapo atasikia msanii wa hip hop ambaye ni rafiki yake kaamua kufanya muziki wa singeli.
Stamina amesema ingawa kila mtu ana shabaha zake katika muziki anaofanya, ila akisikia rafiki yake wa karibu kafanya singeli si kitu ambacho kitamfanya ajisikie vizuri.
“Nakuwa sifikirii poa kwa sababu naona mchizi ni mtu fulani wa harakati fulani lakini inakuwaje hivi tena, lakini kila mtu ana focus yake anapotoa muziki wake kwa hiyo kama yeye ameona sasa hivi soko lipo kwenye mchiriku mimi nitasema dah!!,” Stamina ameiambia Landa 3600 ya E FM na kuongeza.
“Kila mtu ana focus yake katika muziki ndio maana kuna mtu mwingine anajali pesa zaidi, yeye yupo radhi upepo ukihamia kwenye mdumange, anapiga mdumange, ukihamia kwenye kiduku anapiga kiduku yaani yeye anafuta soko lakini wapo wengine wanataka soko liwafuate wao,” amemaliza kwa kusema.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top