Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baada ya Dudubaya kumchana Nay wa Mitego kwamba hana uwezo wa kutunga mashairi ya hip hop na wala hana sifa ya kuwa msanii, Nay amesema hana muda wa kumjibu mtu ambaye hajawahi kumzungumzia katika nyimbo zake.
Rapa Nay wa Mitego ameeleza hayo baada ya watu wengi kusuburi katika mitandao ya kijamii ni jambo gani ataweza kujibu kutokana na yale yaliyozungumzwa na  Dudubaya ambaye anasifika kwa ubabe na utemi.
"Mtu ambaye hajahusika katika wimbo wangu sina muda wa kujibu wala kumzungumzia kabisa sina hiyo 'time", amesema Nay.
Katika hatua nyingine, Nay amesema hana ugomvi wowote na msanii mwenzake Godzilla kwa madai alichokiandika katika ukurasa wake wa Instagram alikuwa anataka kumuelekeza baadhi ya mambo.
"Sidhani kama tuna ugomvi na King Zilla na unaweza kumuelekeza mtu kitu au ukamkosoa kupitia muziki so mimi sina ugomvi na Godzilla labda kama yeye ana ugomvi na mimi na nadhani haiwezi kuwa hivyo, Zilla ni mshkaji hatujawahi kuwa na ugomvi, huwa tunazungumza na nimetoa mtazamo wangu na yeye amejibu kutokana mtazamo wake anavyoona kupitia twitter yake", amesisitiza Nay.
Nay amebainisha hayo baada ya Godzilla kukataa kufanya naye nyimbo ya mabishano baina ya yao.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top