Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa hip hop Bongo, Chemical amedai kitu kilichomfikisha hapo alipo kwa sasa ni kuamini katika uwezo wake.
Chemical amesema ana kila sababu ya kujivunia alipo kwa sasa kutokana muziki anaofanya wapo wanawake wachache sana kutokana na wengi kushindwa kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo lakini yeye ameweza.
“Kuna kipindi cha mwanzo watu walikuwa hawaamini kama naweza kufanya kitu fulani, nimenda kwenye studio kubwa unaishia mlangoni, mtu anakuambia huwezi hata nafasi ya kukusikiliza hakupi, hivyo kuna vitu vingine vinakuwa vinakukatisha tamaa,” Chemical ameiambia E FM.
Pia ameongeza katika kutafuta msaada wa kutoka kimuziki aliweza kukutana na watu wa aina tofauti tofauti ambao kuna wazuri na wabaya pia.
“Kuna ile mtu anakusaidia lakini unakuta anataka kitu kingine, lakini mimi nilikuwa naamini kama mtu anataka kukusaidia sio lazima mimi nitoe kitu, iwe mwili ama mapenzi. Niliamini katika uwezo wangu na nikiamini kama Mungu kaamua nisikike nitatoka,” amesema Chemical.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top