Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amezitaka Asasi za Kiraia (NGO’s) kufungua shule kwa wanafunzi wanaopata mimba shuleni kama kweli zinawapenda wanafunzi hao.
Rais Dkt. John Magufuli
Rais amesema hayo leo Jumanne, Julai 4 alipokuwa akihutubia wananchi wa wilaya ya Sengerema wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji.
“Si kwamba nawachukia wenye mimba, hata kwa bahati mbaya akapata mimba, kama hizo NGO zinawatetea sana, zifungue shule za wenye mimba, kwa sababu zinawapenda wenye mimba, wafungue shule zao,”amesema Rais Magufuli huku akiendelea kusisitiza kuwa.

“Haiwezekani fedha za walipa kodi, Sh 17 bilioni kila mwaka za kusomesha watoto wetu, kwenda kusomesha wakinamama, wazunguke, waimbe, waseme nini mimi ndiyo Rais, huo ndio ukweli,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo Rais Magufuli tatizo si wanaopata mimba, kwani wapo waliopata matatizo, kama kuugua kwa muda mrefu wakashindwa kwenda shule lakini ulianzishwa mpango maalum wa kuwasomesha katika mfumo usio rasmi.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top