Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Prof. Jay akimpandisha jukwaani mkewe, Grace Mgonjo, tayari kwa kumtambulisha kwa wapiga kura wake Mikumi, Morogoro leo katika sherehe iliyofanyika uwanja wa Bustani.
MBUNGE wa jimbo la Mikumi Joseph Haule Profesa Jay leo yupo jimboni kwake Mikumi kwa ajili ya kusherehekea ndoa yake na wananchi wa jimbo lake baada ya wiki iliyopita kufunga pingu za maisha katika kanisa la St Joseph jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali, akiwatambulisha Prof. Jay na mkewe kwa wapiga kura wake.
Katika kuonyesha ni namna gani ana mapenzi na wapiga kura wake wa Mikumi, leo ameamua kufanya sherehe nyingine baada ya ile ya Mlimani City Dar.
Prof. Jay alipowasili kwenye uwanja wa Bustani.
Profesa Jay anafanya sherehe hii ya wazi kwenye uwanja wa Bustani na wakati stori hii inaandikwa kuna gari zima la Coca Cola ambalo lipo mahususi kwa ajili ya kuwagawia soda wakazi wote wa Mikumi waliojitokeza uwanjani hapa.


Mbali na soda, Jay amewaandalia chakula cha kutosha ambacho wote watakaotaka kujumuika naye watakula kadiri wawezavyo.


Wananchi waliohudhuria shughuli hiyo.
Mkewe akiwasalimia wapiga kura wa mumewe.
Msanii wa Singeli, Msagasumu, akitoa burudani kwa wananchi wa Mikumi.
Msanii wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’ akitoa burudani.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top