Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona Neymar anetajwa na jarida la Forbes kuwa mchezaji anayeingiza fedha nyingi zaidi kwa wanamichezo waliochini ya umri wa miaka 25.
Neymar, ambaye atatimiza miaka 26 February 2018, ameingiza kiasi cha $37m, mbele ya mcheza golf Jordan Spieth ($34.5m) na wachezaji wa NBA Kyrie Irving ($29.9m) na Anthony Davis ($28.1m).Mbrazil huyo alisaini mkataba mpya wa kiaka 5 na Barcelona ambao una thamani ya $15m kwa mwaka, lakini pia Neymar anaripotiwa kuingiza fedha nyingi zaidi kutokana na mapato ya matangazo ya biashara.Neymar ndio mwanasoka pekee ambaye anaingiza fedha nyingi zaidi nje ya uwanja kuliko anazopata kutokana na soka moja kwa moja kupitia mikataba yake na Nike, Gillette, Panasonic na Beats by Dre.
Katika listi ya wanamichezo walioingiza fedha nyungi zaidi kwa ujumla – Neymar anashika nafasi ya 18 kati ya wana michezo 100.
Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top