Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mzeze mwenye umri wa miaka 80, Kofi Asilenu raia wa Ghana ambaye ana watoto 100 amedai bado anahitaji kuongeza watoto wawili katika familia yake.
Asilenu ana wake 12 na anaishi na familia yake katika kijiji cha Amankrom kilicho umbali wa kilomita 45 kutoka mji mkuu wa nchii hiyo, Acca. Familia yake ni thuluthi moja ya watu 600 katika kijiji anachoishi.
Sababu ya yeye kutaka kuendelea kuzaa ameeleza kuwa anahitaji familia kubwa kwa sababu hapo awali hakuwa na ndugu, “sina kaka wala shangazi, ndio sababu niliamua kuwa na watoto wengi ili nipate maziko mazuri nikifa,” alisema Asilenu.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top