Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Nuru Hatim akiwa na mwanaye.

Hii ni skendo nzito! Staa mwenye nyota zake wa Afro- Pop, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amekwaa tuhuma nzito, akidaiwa kumpa kibendi mwanamke kutoka Mombasa nchini Kenya aliyejitambulisha kwa jina la Nuru Hatim.
Nuru alitinga jijini Dar wiki iliyopita akitokea Mombasa, Kenya, lengo likiwa ni moja tu, kumpata mzazi mwenzake, Kiba.
Kwa mujibu wa chanzo ambacho kililijua kwa undani saga hilo, Nuru alidai kuwa alikutana na Kiba kwenye shoo nchini humo kasha wakafanya yao na kumuachia kibendi ambacho matokeo yake ni kichanga alichojifungua chenye umri wa miezi mitatu.
ATINGA DAR
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Alhamisi mwishoni mwa wiki iliyopita, Nuru alitinga Dar na kufi ka kwenye Kituo cha Polisi cha Msimbazi- Kariakoo kwa lengo la kusaidiwa kumpata Kiba.
Ilielezwa kuwa, mbali na hilo, pia Nuru alilenga kupata msaada wa kisheria kutokana na msanii huyo kumpa ujauzito na kumtelekeza.

Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, paparazi wetu alifunga safari hadi kituoni hapo ili kuthibitisha hilo, lakini hakufanikiwa kumpata kwa kuwa alikuwa amepelekwa Ubalozi wa Kenya ili aweze kusaidiwa kurudishwa kwao, kwa kuwa hana uwezo wa kifedha kwa sasa.
“Kweli huyo dada alifi ka hapa (Kituo cha Polisi cha Msimbazi), lakini suala lake halikufunguliwa kesi yoyote maana si raia wa hapa.
“Yule mwanamke anadai alikutana na Kiba kwenye shoo ndiyo akanasa kibendi. Pia alikuwa mke wa mtu baada ya kujifungua na mumewe kujua mtoto si wake ndipo ikabidi afunguke kwamba mtoto ni wa Kiba.

ATIMULIWA KWAO
“Kilichofuatia ni kutimuliwa kwao,” alisema sosi wetu ambaye ni miongoni mwa polisi waliokutwa kituoni hapo mchana wa Ijumaa iliyopita.
Baada ya kunasa ubuyu huo, shushushu wetu alifunga safari hadi Ubalozi wa Kenya maeneo ya Oysterbay jijini Dar na kufanikiwa kuzungumza kwa kina na Nuru ambaye alisema kuwa, alifahamiana na Kiba kwa kipindi kirefu lakini wakapotezana baada ya yeye kwenda Dubai kikazi. “Nilipokwenda Dubai, tuliendelea kuwasiliana, akawa ananiambia bado ananipenda sana.

KUVUNJA AMRI YA SITA
“Mwaka jana nilirudi Mombasa na yeye akawa amekuja kufanya shoo Mombasa. Kwa kuwa ninapenda kudensi, alipokuja na mimi nilikwenda kudensi kisha tukaenda kuvunja amri ya sita bila kutumia kinga.
“Nilivutiwa na Kiba kwa sababu ninapenda muziki wake. Niliwahi kushiriki naye tendo mara tatu.
“Hapo mwanzo tulitumia kinga lakini mara ya mwisho tuliona tumezoeana, tusitumie kinga ndipo nikapata mimba na kujua kabisa ni ya kwake kwa hesabu nilizopiga tangu nitembee naye na sikuwa nimefanya ngono na mtu mwingine.HANA NGOMA
“Lakini msimuogope kwa sababu nimepima, sina ngoma,” alisema Nuru huku akiachia tabasamu kwa mbali.
Alisema kuwa, baada ya kunasa kibendi, familia yake ilimjia juu kutaka kujua mhusika ni nani.
“Ilibidi niseme tu kuwa mwenye mzigo ni Kiba. Kilichofuata ni kwamba nilitimuliwa nyumbani, nikaambiwa nimfuate huku ndugu zangu wakinicheka na kuhoji kulikoni kumshobokea msanii wa Bongo.

“Tangu nikiwa na ujauzito, nilifukuzwa, nikawa ninaishi kwa marafi ki, mwisho wa siku na wao wakanichoka na kila nikimtafuta Kiba kwenye simu simpati.
“Ndiyo maana imebidi nije Bongo, nilivyofi ka pale Ubungo (Stendi ya Mabasi ya Mikoani), niliulizia na kuelekezwa hadi kwao.
“Nilipokwenda kuonana na mama yake, alisema Kiba hayupo, amesafiri hivyo nitafute njia ya kurudi kwetu na mimi sina mbele wala nyuma, nimechakaa, sikuwa hivi, nilikuwa mzuri sana, hii ni sababu tu ya ugumu wa maisha, sina hata hela ya maziwa ya mtoto, ninamshukuru Mungu watu wa ubalozi wetu wananisafi risha, ninarudi kwetu,” alisema Nuru.Kutokana na sakata hilo, paparazzi wetu alimvutia waya Kiba ambaye simu yake haikuwa hewani, ndipo akamtafuta meneja wake, Christina Moshi ‘Seven’ ambaye hakuwa tayari kuweka wazi.

KIBA SASA
Kwa upande wake, Kiba, akizungumza na redio moja nchini baada ya kubanwa juu ya skendo hiyo, alijitetea: “Amlete mtoto, kama kuna anaeongea hivyo vitu, unaenda unamsikiliza na mtoto lazima apime damu ‘DNA’ ndiyo kila kitu.”


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top